TTCL

EQUITY

Tuesday, December 15, 2015

Nimetengeneza video 2 sababu ya maadili - Mwana FA

Msanii Mwana FA amesema aliamua kufanya video mbili za wimbo mmoja, baada ya kuwa na mabishano ya muda mrefu na director wa video hizo, kuhusu kipi kitoke na kipi kibaki wakati wa kutengeneza.
 
 
Mwana FA ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kwenye video hiyo kulikuwa na sehemu ambazo zisingefaa kuonyeshwa kwenye runinga za hapa nyumbani, hivyo alitaka sehemu hiyo iondolewe huku director wake akikataa kuziondoa.

“Video ilivyokuja nikamwambia hii video ilivyo local chanel za hapa kwetu haiwezi kuonyeshwa, ikabidi nimwambie sekunde hii mpaka hii utoe, jamaa akabisha kabisa akasema hiyo ndiyo video yenyewe, kwa hiyo atachoweza kufanya ataziondoa zile parts ambazo mimi nimesema, lakini huku ambako ana uhakika video inacheza jinsi ilivyo ataipeleka kama ilivyo, haikuwa lengo langu kutengeneza video mbili ila mazingira yalinipeleka huko”, alisema Mwana FA.

Mwana FA amesema alipopata script ya video hakuwa na taarifa kamili jinsi video hiyo itakavyokuwa, lakini alipoenda kufanya video hiyo ndipo alipokuta hali hiyo ambayo ilimlazimu atengeneze video mbili.

“Mi nililetewa script lakini haikuwa na detais moja kwa moja kwamba watu watakuwa wamevaa nini, wata act vipi, mi mwenyewe ilibidi nisafiri na begi mbili kuhakikisha nina kila kitu ninachokitaka, ulipofika muda ndo nikaona wamevaa hivi, wanakuwa directed wafanye hivi”, alisema Mwana FA.

Pia Mwana FA amesema mara baada ya video hiyo kukamilika itapelekwa kwenye vituo vya televisheni vyote vya hapa ndani na nje, na pia ataiweka you tube ili mtu atakaye taka kuiona ataiangalia humo.

No comments:

Post a Comment