MARA kadhaa migomo
ya wafanyakazi imekuwa ikizaa
athari mbaya kwao. Hii ni kutokana na
kugoma bila kufuata
taratibu. Waajiri wao ni
wajanja. Huwa makini sana linapoibuka wazo
la kugoma na
huwa tayari muda
woote kufuatilia nyendo
ili panapo kosa
kidogo watumie mwanya
huo kuwadhibiti wagomaji.
Na kikubwa wanachofanya hali ikishakuwa
hivi ni kusema
mgomo haukuwa halali
na hapo kupata
nafasi ya kuwashugulikia waliohusika
katika kugoma mmoja baada ya
mwingine. Katika mazingira
kama haya ni
vema wafanyakazi kufahamu
taratibu za kisheria
zinazohusu mgomo ili
wakati wa kufanya
hivyo asitokee yeyote kati
yao wa kuathiriwa
na ugomaji huo.
1. SHERIA INAMRUHUSU
MFANYAKAZI KUGOMA.
Wapo wanaodhani kugoma
ni uasi. Kwa
mfanyakazi hili si
kweli. Kugoma ni
haki ya mfanyakazi kama zilivyo haki nyingine. Kama
ilivyo haki ya
kupokea mshahara, haki ya kulipwa
muda wa ziada, haki
ya muda maalum wa
kufanya kazi, likizo na haki nyinginezo
kwa ujumla wake. Kugoma
si dhambi isipokuwa
takwa halali la
kisheria. Kitaalam mgomo
wa wafanyakazi huitwa
“strikes” . Ni hatua
ambapo wafanyakazi hugomea
kuingia maeneo ya
kazi au huingia
maeneo ya kazi
lakini wasitoe huduma
kama ilivyo ada yao.
Kisheria kugoma ni
jukwaa la kuitisha
mjadala wa kujadii
maslahi ya kazi
kati ya mwajiri
na mwajiriwa. Kugoma
ni Jambo halali
kisheria ndicho ninachotaka
kusema na kuwatoa
hofu baadhi wajuao
kugoma ni uasi
na usaliti.Na haya ni kwa
mujibu wa kanuni namba ya
42,sheria namba 6 ya ajira
na mahusiano kazini.
2. WAFUATAO
HAWARUHUSIWI KUGOMA.
Makundi ya wafanyakazi
watoao huduma muhimu
katika jamii migomo
kwao imeharamishwa. Huduma
muhimu katika jamii
hutegemea na mahitaji
ya jamii husika. Yumkini hapa
kwetu huduma muhimu katika
jamii hujumuisha watumishi katika
idara za afya, maji
safi na salama,
nishati na umeme,
vyombo vya ulinzi
na usalama, zimamoto na watoa
huduma ya kuongoza
ndege. Sababu kubwa
za kuzuia makundi
haya kugoma ni
kuwa kugoma kwao
huweza kuleteleza hasara ambazo
kwazo haziwezi kufidiwa
na kitu chochote
baada ya kutokea kwake. Na hasara
kubwa zaidi hapa ni
vifo na ulemavu
wa kudumu vitu ambavyo
haviwezi kufidiwa kwa
namna yoyote na kitu
chochote .
3. WANAOTAKA
MGOMO HALALI WAFUATE
UTARATIBU HUU.
( a ) Kwanza kabisa
hakikisheni mgomo wenu
unahusu maslahi ya
kazi yenu. Usiwe
mgomo ambao nyuma yake
wako watu hasa wanasiasa wanaowasukma
ili kutimiza haja zao
fulani. Au usiwe mgomo
ambao umeandaliwa lengo
likiwa kumkomoa mwajiri.
Ni lazima kuwepo
na nukta muhimu
na ya wazi
kabisa inayohusu maslahi
katika kazi yenu.
( b ) Kabla ya
kugoma lazima muwe mmepitia hatua
ya usuluhishi( mediation). Na mnapokuwa
mmepitia hatua hii ni
lazima iwe imethibitika
kuwa hatua hiyo
imeshindwa kutatua mgogoro
wenu na sasa
hatua inayofuata ni
ya kugoma. Ikiwa
hatua ya usuluhishi
imefanikiwa na kutoa majawabu
ya mgogoro
itakuwa ni haramu kwa yeyote
kugoma. Kugoma ni pale
tu hatua ya
usuluhishi inaposhindwa na
hatua hii hutakiwa
kuchukua muda wa
siku thelathini. Ni muda
huo utakaotumika kutafuta muafaka
kabla ya kutangaza
mgomo.
( c ) Ikiwa mgomo
utakuwa umeitishwa na
chama cha wafanyakazi
basi kura za wengi
ndizo zitakazotoa ruhusa
ya kugoma. Ikiwa wengi
watakataa basi hakuna
mgomo.
( d ) Baada ya usuluhishi
kushindikana wafanyakazi wanaolenga
kugoma watatakiwa kutoa
taarifa(notice) ya masaa
48 sawa na
siku mbili kwa mwajiri
kabla ya kuanza kugoma. Ni baada ya
muda huo ndipo mgomo
utaanza.
( e ) Ikiwa mgomo utaahirishwa
baada ya masaa
48 yaliyokuwa yametangazwa
kupita, basi kama
mnatarajia kuendelea na
msimamo wa kugoma
mtatakiwa kutoa muda mwingine
wa masaa 48.
Kama wafanyakazi
watafuata utaratibu huu
kugoma hakuna madhara
yoyote mabaya yatakayotokea kwao ikiwa
ni pamoja na
kutishiwa kufukuzwa kazi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
MAGAZETI YA HABARI LEO, JAMHURI, NA NIPASHE.
simu; 0784482959, 0714047241 au barua pepe; bashiryakub@ymail.com
No comments:
Post a Comment