Zaidi ya vijana 30 kutoka katika vyuo mbalimbali
mkoani Mtwara wamepatiwa elimu juu ya masuala ya uwekezaji katika
rasilimali za Mafuta na Gesi asilia, katika semina ya siku moja
iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la MRENGO.
Baadhi ya mitambo katika Kituo cha Kupokelea Gesi Asilia kutoka
Songosongo na Mtwara kilichopo Somangafungu wilayani Kilwa Mkoani Lindi
Wakizungumza
mara baada ya kumalizika kwa semina hiyo, baadhi ya wanafunzi hao
wamesema imewasaidia kuweza kufahamu mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na
namna rasilimali hizo zitakavyoanza kuwanufaisha wananchi ambao wengi
wao wanatarajia kuona mafanikio kwa siku za karibuni.
Kwa upande wake, mratibu wa mradi wa Mafuta na Gesi unaotekelezwa na shirika hilo kwa kufadhiliwa na shirika la Utunzaji wa Mazingira Duniani (WWF), Mustafa Kwiyunga, amesema lengo la kuwajengea uwezo vijana hao ni kutaka kuendeleza majadiliano hasa katika vyuo mbalimbali na pia waende kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu juu ya rasilimali hizo kwa wananchi.
Naye, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Maris (STEMMUCO) mkoani Mtwara, Justin Lusasi, amewataka wazizi na walezi kuhamasika katika kuwapeleka shule watoto wao kwa ajili kuwatengenezea misingi bora ya maisha ambayo wataipata kupitia rasilimali hizo, na waache kupoteza muda katika masuala ya Jando na Unyago.

No comments:
Post a Comment