Mkuu
wa Mkoa Kilimanjaro Amos Makalla mwenye miwani akizindua huduma ya maji
katika kijiji cha Mabogini, mkoani Kilimanjaro wenye thamani ya Sh
Milioni 343.
ZAIDI
ya wananchi 3000 wa kijiji cha Mabogini, kitongoji cha Shabaha, mkoani
Kilimanjaro, watanufaika na huduma ya maji safi na salama, baada ya
kupelekewa mradi wenye thamani ya Sh Milioni 343. Mradi huo
uliozinduliwa jana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla,
umesimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi Moshi (MUASA), ukiwa na lengo la
kuwapatia huduma bora ya maji wakazi katika kijiji hicho.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, RC Makalla aliwataka wananchi kutunza mazingira na
kulinda vyanzo vya maji, bila kusahau upandaji wa miti ili wasiharibu
vyanzo vya maji. Alisema bila hivyo hali ya maji katika maeneo hayo
itakuwa ngumu, hivyo kuna kila sababu ya wananchi hao kuielewa na
kuiabudu sera ya utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti katika maeneo
yao. “Naomba wananchi tulinde miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha
kwamba miradi ya maji inakuwa endelevu katika maeneo yetu tunayoishi,
maana maji ni uhai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla akimtwishwa ndoo ya maji mkazi
wa kijiji cha Mabogini baada ya uzinduzi wa mradi maji katika eneo
hilo.
Mazungumzo yanaendelea katika uzinduzi huo wa maji.
RC Kilimanjaro Amos Makalla akifungua maji kama ishara ya kuzindua rasmi mradi huo.
RC
Kilimanjaro Amos Makalla wa nne kutoka kushoto waliokaa akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali mkoani Kilimanjaro na
watendaji wa MUASA.
“Tunaamini tukiamua kwa pamoja
kufuata maelekezo ya wataalaamu juu ya utunzaji wa mazingira tutaishi
vizuri na huduma ya maji itapatikana kwa urahisi,” alisema RC Makalla.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa
Mkoa Kilimanjaro, Amos Makalla, amekabidhi hundi yenye thamani ya Sh
Milioni 100 kwa vikundi 45 kwa Halmashauri ya Moshi, huku vikundi hivyo
vikiwa ni 39 vya akina mama na 6 kwa vijana. Fedha hizo ni utekelezaji
wa maelekezo ya serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato
ya ndani kutoa mikopo kwa akina mama na vijana.
RC Makalla ni miongoni mwa
viongozi wa serikali wanaokwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu inayoendeshwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli,
akisimamia na kuzunguuka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro
kwa ajili ya kufanikisha maendeleo ya wananchi wake.
No comments:
Post a Comment