Meneja Mkazi wa kampuni ya JovagoTanzania, Bw. Andrea Guzzoni.
“Maendeleo ndani ya sekta ya Utalii hayawezi kufikia kiwango nzuri iwapo hakutakuwa na wafanyakazi wenye ujuzi wa kutosha”
Kukua kwa
sekta ya utalii kunategemea hudumu za ukarimu kwa kiasi kikubwa. Huduma
hizi zinapaswa kufanywa na wajuzi waliobobea ndani ya sekta ili kuweza
kuwaridhisha wageni na kuleta maendeleo katika soko hili la utalii.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mkazi wa kampuni ya
JovagoTanzania, Bw. Andrea Guzzoni alifafanua kuwa, ukarimu na ujuzi
wa kutosha kwa wahudumu wa mahotelini na sekta malimbali za utalii ni
jambo muhimu kwa kuwa litaongeza pato la taifa kutokana na ongezeko la
wageni watao hitaji huduma hizo bora na zenye viwango .
“Watanzania
inabidi tufahamu kuwa kila mtu akiwa nje ya eneo la nyumbani kwake
atahitaji apate huduma kama ya nyumbani kwake au na zaidi, hivyo
tuzingatie matuzi ya lugha nzuri, na huduma za viwango vinavyotakiwa”.
Aliongezea kwa kufafanua kuwa, “Hata
hivyo bado hoteli nyingi zinaajiri wafanyakai wasio na elimu ya
kutosha, wafanyakazi ndani ya sekta hii wanatakiwa kujua lugha zaidi ya
mbili ikiwemo lugha za kimataifa, lakini kwa Tanzania wahudumu wengi
hawafamu lugha hii ya kigeni na kumpa shida mtalii wa nje”
Tutambue
kuwa huduma ndani ya sekta ya utalii au mahotelini haziwezi
kuwaridhisha watalii kwa njia za mashine bali watu wenyewe. Hivyo
Wafanyakazi wana nafasi kubwa katika kukuza sekta hii ukiringanisha na
sekta nyingine zinazoweza kutendeka bila ya nguvu kazi za watu.
Kwa upande
wake, Bw. Richard Rugumbana wa Tourism Confederation of Tanzania (TCT)
alifafanua kuwa “Serikali pamoja na sekta binafsi tujitahidi kutilia
mkazo kuongeza mafunzo ya ziada ya taaluma ya utalii, “Ni vizuri
tukajifunza mafunzo ya ndani na nje ya nchi yaliyobobea, pia tuweke
utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wafanyakazi tuliowaajiri na kuwapa
vipaumbele kwa wafanyakazi wenye elimu ya juu kama kuwapa vipato
vinavyoendana na elimu yao. ”
No comments:
Post a Comment