STAA wa filamu Bongo, Flora Mvungi na shostito wake, Riyama
Ally juzikati walijikuta wakigeuka kivutio ukumbini baada ya kufunikana
kwa kuzikata nyonga bila aibu kwenye hafla ya kumpongeza mtoto wa Flora,
Tanzanite Hamis kuchaguliwa kuwa balozi wa duka la kuuza nguo.
Flora Mvungi.
Rihama Ally.
Tukio
hilo lilitokea hivi karibuni Hoteli ya City Style Sinza-Mugabe jijini
Dar es Salaam, ambapo wawili hao walivamia katikati ya ukumbi na kuanza
kushindana kuzungusha nyonga hadi kufikia hatua ya kuacha kucheza wakiwa
wamesimama na kuamua kulala chini.
“Jamani huyu si Riyama na yule aliyelala ni Flora, mhhh wanajua kuzikata,” ilisikika sauti ya mhudhuriaji ukumbini hapo.
No comments:
Post a Comment