Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste katika Kijiji cha
Itaga mkoani Singida, David Mtipa (59) na mkewe, Maria Phillip (45),
wanasota katika Gereza la Singida baada ya kushindwa masharti ya dhamana
kufuatia kufikishwa mahakamani Ijumaa iliyopita kwa madai ya kumfungia
ndani kwa miaka 12, mtoto wao, Timotheo (30).
Timotheo anayedaiwa kufungiwa ndani na wazazi wake kwa miaka 12. |
Watuhimiwa hao walipandishwa kizimbani kwa madai ya kushindwa
kumpatia huduma muhimu mtoto huyo kwa kipindi cha miaka 12, tangu akiwa
na umri wa miaka 18.
Mwanasheria wa Serikali, Patrisha Mkina alidai mbele ya Hakimu
Mwandamizi wa Mahakama ya Singida, Faisal Kahamba kuwa, kati ya mwaka
2003 mpaka 2015, kwa makusudi, Mchungaji David akishirikiana na mkewe
Maria walishindwa kumpatia Timotheo huduma muhimu za kibinadamu.
“Wanandoa hao walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria,” alisema mwanasheria huyo.
Alisema
kwa miaka 12, washitakiwa walimnyima Timotheo malazi, chakula, nguo,
matibabu na uhuru wa kikatiba kitendo ambacho kimechangia apate madhara
ya kudumu ya afya.
Washitakiwa walikana mashitaka hayo na kesi hiyo itatajwa tena,
Desemba 28, mwaka huu. Washitakiwa walipewa masharti ya dhamana ya
wadhamini wawili ambao wangeweka dhamana ya shilingi milioni moja kila
mmoja, wakashindwa kutimiza.
Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi mkoani Singida lilimshikilia
nchungaji huyo na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani kwa miaka 12 mtoto
huyo mwenye ulemavu wa viungo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Tobias Sedoyeka alisema tukio
hilo la kusikitisha liligunduliwa na wasamaria wema ambao walitoa
taarifa serikalini.
Kamanda Sedoyeka alisema Timotheo alikuwa akipata huduma zote chumbani zikiwemo chakula, haja ndogo na kubwa.
Kamanda Sedoyeka alisema Timotheo alikuwa akipata huduma zote chumbani zikiwemo chakula, haja ndogo na kubwa.
“Wazazi hao walisema, kijana wao alizaliwa mwaka 1984 akiwa mzima.
Akiwa darasa la 6, mwaka 2003, alianza kuugua ugonjwa usiojulikana,
akawa anaanguka na kutoa povu mdomoni huku mwili wake ukibadilika rangi
kuwa wa njano na akatibiwa bila mafanikio.
“Walisema baada ya Timotheo kutibiwa bila mafanikio, ndipo wao
waliamua kumfungia ndani wakiona kuonekana kwake mitaani
kunawafedhehesha katika jamii,” alisema.
No comments:
Post a Comment