Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Juma, mkazi wa Tegeta A, Dar amejikuta akikamuliwa faini ya Sh. laki tano kufuatia kufumwa ugoni na mke wa mtu.
Katika tukio hilo lililojiri Kimara-King’ong’o, Dar, Jumapili iliyopita, Juma alifumaniwa na mke wa mwanaume aitwaye Swai aliyetajwa kwa jina moja la Cesilia, mkazi wa maeneo hayo.
Ilidaiwa kuwa Cesilia alimwachia mumewe mtoto na kumuaga kuwa anakwenda harusini ambapo mumewe alimkubalia bila kujua kumbe anakwenda kuzini.
Ilisemekana kuwa muda mfupi baadaye, kuna vijana walimfuata Swai na kummwagia ‘upupu’ kuwa mkewe alikuwa akisaliti ndoa yao.
Ilifahamika kuwa vijana hao walimchukua Swai na kumpeleka hadi kwenye nyumba ambayo wenyewe hawajahamia iliyopo karibu na biashara yao ya duka ambapo baada ya mwenye mali kuingia, alimkuta Juma akiwa amevaa ‘singlendi’ na bukta ambapo alizidi kuangaza macho huku na kule ili amuone mkewe.
Ilidaiwa kuwa alipomaliza kukagua kila ‘engo’ ndani ya nyumba hiyo aliingia chooni ndipo akamkuta mkewe akiwa amejificha chini ya ‘sinki’ la choo.
Iliendelea kusemekana kuwa baada ya kumuona mkewe, Swai alimnyanyua na kumuuliza kulikoni lakini hakuweza kumjibu.
Ilidaiwa kuwa Swai aliwaacha wawili hao ndani na kuwafungia ambapo alitoa taarifa kwa mjumbe wa eneo hilo, Zakaria ambaye alifika eneo la tukio mara moja huku akifuatiwa na Mtendaji wa Serikali za Mitaa, Amina Rashid.
Ilielezwa kuwa viongozi hao walipofika walikuta umati mkubwa umejaa uliotaka kujua hatima ya tukio hilo hivyo ilibidi watoe taarifa polisi ambao walifika mara moja na kuwachukua watuhumiwa huku wakisindikizwa na kadamnasi hadi Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar.
Habari za kipolisi zilieleza kuwa wakiwa kituoni hapo, Swai alimwekea dhamana mkewe huku Juma akibaki ‘lokapu’ hadi alipokwenda kuchukuliwa na mwenyekiti na mjumbe wa mtaa kwani kesi hiyo ilirudishwa kwenye ngazi ya kijiji ili wazungumze na kuyamaliza.
Viongozi wote walikiri kuwa walizungumza suala hilo wakiwa na mwenye mke ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa Juma amlipe Swai Sh. laki tano kama faini au adhabu kwa kosa alilotenda.
Ilielezwa kuwa Juma hakuwa na kiasi hicho cha fedha hivyo aliwekewa dhamana na ndugu yake na kuahidi kulipa mwezi wa kumi, mwaka huu.
Kwa upande wake, Swai alisema kuwa ameamua kumrudisha mkewe kijijini kwao kwa miezi kadhaa au mwaka mmoja huko Rombo, Moshi mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya adhabu yake.
Kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo, awali Juma alifunguliwa jalada la kesi katika Kituo cha Polisi cha Kimara-Temboni namba KM/RB/2931/13 TAARIFA alikolala kwa siku moja.
No comments:
Post a Comment