Frank
Mvungi
Maafisa
Maendeleo ya jamii walioajiriwa katika Halmashauri hapa nchini wameongezeka kutoka 1,855 mwaka 2005
hadi kufikia 2,675 ikiwa ni ongezeko la asilimia 44 hali inayosaidia kuboreshwa
kwa huduma za jamii.
Kauli hiyo
imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia vyuo
vya Maendeleo ya Jamii Bi. Neema Ndoboka toka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wanawake Wazee na Watoto wakati wa Mkutano na Vyombo vya Habari
uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa na Wizara hiyo katika kukuza Sekta ya
Maendeleo ya Jamii hapa nchini.
Ndomboka amesema kuwa, chuo cha Maendeleo ya jamii Tengeru kimepandishwa hadhi kuwa Taasisi ya Elimu ya Juu inayojitegemea
kiutendaji, hali itakayosaidia kuongeza kiwango wa Maafisa Maendeleo ya Jamii
wanaohitimu katika chuo hicho.
Pia Ndomboka
amesema kuwa vyuo vinavyosimamiwa na Wizara hiyo vinatoa wahitimu wanaokidhi
mahitaji ya soko la ajira kutokana na umahiri na uzoefu wanaojengewa wakiwa
vyuoni.
Aidha
wahitimu wa Kidato cha nne na kidato cha sita wenye utashi katika fani ya
maendeleo ya jamii wanakaribishwa kutuma maombi yao kwenye “Central Admission
System” (CAS), kupitia www.nacte.go.tz
Taaluma ya
Maendeleo ya Jamii inatolewa kwa kuzingatia taratibu na Kanuni zinazotolewa na
kusimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). hivyo NACTE inasimamia
uandaaji wa mitaala inayotumika katika utoaji wa mafunzo, muda wa
masomo,mitihani na Vigezo vyake, pamoja na ubora wav yeti wanavyotunukiwa
wahitimu kwa kila ngazi.
No comments:
Post a Comment