Zimamoto wakijaribu kupambana na vifaa vyao kwaajili ya kuuzima moto huo.
Ofisi za Kliniki ya afya ya mapenzi iliyopo jijini Mwanza karibu na
jengo la Nyanza leo majira ya saa tisa alasiri imeungua moto na
kuteketeza vitu mbalimbali vilivyokuwepo katika kliniki hiyo.
Wakizungumza na www.globalpublishers.co.tz mashuhuda wa tukio hilo
wamesema waliona moshi ukitoka katika ofisi hizo na kutoa taarifa kwa
jeshi la zimamoto ambalo liliwahi kufika katika eneo la tukio lakini
walitumia muda mrefu kufunga bomba la kurushia maji jambo
lililosababisha kuungua kwa vifaa vingi vya ofisi hiyo.
Kwa upande wake, mmiliki wa kliniki hiyo, Paul Nelson amesema wakati
tukio hilo linatokea yeye alikuwa Mwanza Hotel iliyopo karibu na ofisi
hiyo na aliona moshi mkubwa ukitoka katika ofisi yake na kutoa taarifa
kwa zimamoto.
Nelson amesema chanzo cha moto huo kimenatokana na shoti ya jenereta
lililokuwa limewashwa kutokana na kukatika kwa umeme na jenereta hilo
lilikuwa halitumiki kwa muda mrefu jambo ambalo limefanya kutokea kwa
shoti hiyo na kusababisha moto mkali uliounguza ofisi yake.
Alivitaja vifaa vilivyoungua kuwa ni pamoja na laptop yenye thamani
ya shilingi laki nane (800,000/=), simu mbili pamoja na mafaili
aliyokuwa anayatumia katika ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment