Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa taarifa
kuhusu uhalali wa filamu ya Mapenzi ya Mungu kama ni halali kumilikiwa
na Elizabeth Michael ‘Lulu’ kufuatia kuwepo kwa maneno kuwa hakustahili
kutwaa tuzo ya African Magic Views Choice Award (AMVCA) sababu filamu
hiyo haikuwa na umiliki wake.
Katika
taarifa hiyo imeeleza kuwa kuhusishwa kwa watu mbalimbali katika
utengenezaji wa filamu hakuwezi kubadili uhalali wa filamu na
kudhibitisha kuwa filamu hiyo inamilikiwa kihalali la Lulu.
“Ili
filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa
kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika
mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.
“Tunapenda
kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya Mungu ni
Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani ana haki
zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo,” ilieleza
taarifa hiyo.
Aidha
taarifa hiyo iliongeza kuwa filamu hiyo ilitengenezwa na kampuni ya
Proin Promotion na ilisajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.
No comments:
Post a Comment