TTCL

EQUITY

Thursday, December 3, 2015

Kortini kwa kutishia kumuua 'Damian Lubuva'




WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kula njama ya kuua mtu aliyetajwa kwa jina jina la Damiani Lubuva na familia yake, kinyume na kanuni ya sheria ya adhabu kifungu 215 sura 6 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Wakisomewa mashataka hayo jana na Wakili wa Serikali Hellen Moshi, ilidaiwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Thomas Simba, kwamba watuhumu walitenda kosa hilo Oktoba 25 na Novemba 16, mwaka huu.

Alidai mahakama hapo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walikula njama kutaka kumuua mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Damian Lubuva na familia yake.

Wakili Moshi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Samwel Gigaru (30) ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Kipunguni Ukonga na mtuhumiwa wa pili ni Angela Mbonde (36) Mwanasheria, Mkazi wa Sinza. Watuhumiwa hao walikana shtaka hilo na kurudishwa rumande hadi Desemba 15, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena. Wakili wa upande wa watuhumiwa, Moses Kaluwa,aliiomba mahakama iwapatie wateja wake dhamana.

Hata hivyo, wakili Moshi alipinga ombi hilo kutokana na ualisia wa kosa, hivyo aliitaka Mahakama iwanyime dhamana kwa muda kutokana na kesi hiyo kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Hakimu Simba, alisema washtakiwa wana haki ya kupata dhamana, lakini kutoka na asili ya kosa inabidi warudishwe rumande. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa. 

No comments:

Post a Comment