Mimi
ni mpenzi sana wa semina za Dk. Ndodi ambaye hutoa elimu juu ya mambo
mbalimbali ikiwemo elimu juu ya lishe bora ambayo hutoa mara kwa mara
katika vyombo vya habari. Siku moja nilimsikia akisema kuwa panya
wanamzidi binadamu akili kwa sababu katika mbegu za mahindi huwa anakula
viini vya ndani vya njano ambavyo ni sehemu mzuri katika mahindi. Cha
kustaajabisha, binadamu anayejiita mwenye akili kuliko viumbe wote
anavitoa viini hivyo kabla ya kuyasaga hayo mahindi ili kupata unga wa
ugali!!!!!
Msemo
wa Dk. Ndodi ninauunga mkono kwa asilimia 100 kwani nimegundua si
Watanzania peke yake wanazidiwa akili na wanyama, ndege na wadudu bali
hata wazungu nao wamelidhihirisha hili kwa sasa. Haiwezekani na
haijawahi kutokea kuwa wanyama, wadudu, na ndege wenye jinsia moja
wametakana kimapenzi. Ikitokea umemuona jogoo akimpanda jogoo mwenzake
ama temba anampanda temba mwenzake, jua dunia imefika mwisho.
Binafsi
ninasikitishwa sana na kitendo cha wazungu kuhimiza kukubalika kwa ndoa
za jinsia moja – eti wanaume waruhusiwe kuoana na wanaume wenzao na
wanawake pia waoane na wanawake wenzao! Hili linadhihirisha kuwa
binaadamu hawana akili…
Kwa
sasa nimeanza kutilia mashaka ule msemo wa kuwa binadamu ndiye kiumbe
mwenye akili kuliko viumbe wote. Hatuwezi kusema hivyo tena kutokana na
mambo ya kipuuzi tunayoyafanya na kuyashadadia, na ambayo hayajawahi
kufanywa na mnyama, ndege ama mdudu yeyote ingawa tunadai kuwa hawana
akili.
Vitabu
vya dini vinatuambia kuwa Mungu alituleta duniani ili tuoane na
kuongeza dunia kwa kuzaa binadamu wengine. Sasa swali langu litabakia
palepale kuwa watoto watatoka wapi ikiwa wanaume kwa wanaume na wanawake
kwa wanawake wanaoana, na hili limehalalishwa duniani kote na Mabepari
wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini?
Na
ukumbuke katika vitabu hivyo hivyo vya dini, Mungu aliwaadhibu vikali
Wasodoma na Wagomora walioyafanya haya haya ambayo kwa sasa
yamehalalishwa. Hili linadhihirisha ni makosa makubwa sana.
Nina
kuhakikishia itafika kipindi sheria itaanza kutetea wazee wanaowabaka
watoto wao kwa msemo huo huo “ Uhuru na Haki za Binadamu
Mdau, unalizungumziaje hili suala wewe???
No comments:
Post a Comment