Inakuwa nene masela wangu? Kipande hii ni mzuksi kichizi arifu. Kama vipi welikamu kwa sana kwa fasi ya hapa jamvini tukisanue mazee ama nini! Basi sawa.
Wanangu kuna ishu zingine hazihitaji mtu
kuwa machi noo kozi kuna pipo ni mamasta maindi ileile na ukileta za
kujua sana dheni watu wanakupiga chabo dheni wanakuchora tu si unajua
zile? Kuna wale makaksi wa ukwehe ambao mara nyingi siyo wachangiaji wa
mamada kiivo bati wana madini ile mbaya kwa kichwani! Ebana kitu cha
holidei ya uhuu vepe? Mambo ya foto kanga na ekotite yalikuwa mpango
mzima? Barida!
Basi bana huku na huku selaa wangu
akamingo na chiki mmoko mkare aibu kiaje sasa mazee. Yaani usipimie
kabisa kwa jentromani wa ukwehe achana na wale watoto mayai lazima uzime
fegi kachala wangu.
Siyo siri wanangu mtoto ni sumu ile
mbaya sema tu laifu lake huko nyuma lilikuwa la kukurukakara za hapa na
pale wanangu wenyewe kwenye mambo yaleee ya kubadili mameni kama chizi
f’lani hivi freshi.
Laifu limemuvu fasta na huwezi kubilivu
si ndo msimu wa kitu cha holidei? Masela hii siyo taimu ya kumbwela ni
mwendo wa maandalizi ya kufa mtu ili wanangu wasiaibike.
Unaambiwa jamaa yangu kazama ofisini kwa
shori hapo dauni tauni Bongo tambarare kupata sevisi f’lani si ndo
kachaa kadata na mtoto? Akaona isiwe kitu, baada ya kitambo f’lani hivi
mwana akatangaza kuweka kitu na boksi ndani.
Sasa bana unajua ukitaka kugonga bata la
holidei usimchunguze sana kozi hutalila kwa raha au hutalila kabisa.
Basi bana, kabla ya kumweka kwa skani akaona amwekee spai wa kumchunguza
kama ametulia au ndo kama hivo magumashi?
Yule msela aliyepandikizwa na mwana si
ndo akaanza mbishe za kumfukuzia shori? Kama nilivyokuteli bifoo kwamba
tabia ni kama rangi kuifuta ina kosti zake. Jamaa kamuimbisha shori hadi
wakakubaliana wakafanye yao kwa hoteli!
Da! Noma sana wanangu! Shori amefika kwa mapokezi kakaribishwa freshi na bashasha za kumwaga kisha akapewa funguo za rumu.
Mazee wakati shori anamsikilizia jamaa
akiwa amejimwaga kwenye peji ndani ya suti ya kuzaliwa, ghafla bin vuu
mlango ukagongwa…kwenda kufungua shori hakuamini macho yake kukutana
feisi kwa feisi na mchumba’ke orijino kumbe alikuwa amechezewa maindi
tu.
Mnanyaka masela unajua kwenye hili laifu
siyo ishu kuringia uzuri na kushindwa kujikontroo. Ni beta mazee mtu
ukaringia bahati na siyo kitu cha sura na umbo bomba.
Ona sasa, pamoja na ukare wa shori bati kitu cha uchumba mwisho wa reli na laifu limestaki.
No comments:
Post a Comment