Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Aisha madinda ambae jina lake halisi ni Aisha Mbegu alizaliwa mwaka 1980 katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar na alipata umaarufu mkubwa kwa uhodari wake wakucheza muziki alipokuwa kwenye Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta"
Vile vile Aisha aliwahi kuingia kwenye tasnia hii ya filamu na kuweza kuigiza filamu na watu kama aliekuwa muimbaji wa Bendi ya Msondo, TX Moshi William (Marehemu) pamoja na mcheza soka Boniphace Pawasa.
Taarifa zaidi juu ya msiba huu tutaendelea kukujuza kadri tutakapo pata taarifa.
Pole ziende kwa ndugu na jamaa na wote walioguswa na msiba huu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema pemoni AMEN.
No comments:
Post a Comment