Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akipata maelezo mara baada ya
kuwasili kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Kutoka
kushoto ni Mgeni rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa, Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama pamoja na Mkuu wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali, Elias Athanas wakitoa heshima kwa
wimbo wa taifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akizungumza kwenye maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei,
2016.
Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akisoma hotuba pamoja na ujumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Ban Ki-Moon kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye
Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mgeni
rasmi Meja Jenerali James Mwakibolwa akiweka shada la maua kwenye mnara
wa mashujaa kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa walipoteza
maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine yenye machafuko
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa
Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mkuu
wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Meja Jenerali, Elias Athanas akiweka shada la maua kwenye mnara wa
mashujaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Mwakilishi
Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama akiweka shada la maua kwenye mnara wa mashujaa kuwakumbuka
Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha katika oparesheni
ya kulinda amani katika nchi zenye machafuko wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika
kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei,
2016.
Mkuu
wa Jeshi la Akiba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Meja Jenerali, Elias Athanas akisalimiana na Mwakilishi Msaidizi Mkazi
wa Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama mara
baada ya kuwasili katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda
Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016. Katikati ni Afisa Habari
wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.
Brass
Band ikiongoza gwaride maalum la askari walinda Amani kuingia viwanja
wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa
Mataifa katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31
Mei, 2016.
Baadhi
ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Balozi wa nchi mbalimbali
pamoja na viongozi wa Dini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku
ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kwenye
Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 31 Mei, 2016.
Na Mwandishi wetu
Katika
kutambua kujitolea kwa Tanzania kutoa askari wake kwenda kulinda amani
katika nchi zingine, Umoja wa Mataifa (UN) umesema unatambua huduma
inayotolewa na Tanzania ikiwa kama mwanachama wa UN na unafurahishwa na
hatua iliyopo ya kuendelea kusaidia kulinda amani katika operesheni
zinazofuatia.
Hayo
yamesemwa na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa
ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ambapo kwa nchini siku hiyo
iliadhimishwa Dar es Salaam katika Uwanja wa Mashujaa wa Mnazi Mmoja
Manyama
alisema Tanzania imekuwa ikijitolea kusaidia ulinzi wa amani katika
mataifa mengine licha ya kupoteza baadhi ya wanajeshi wake lakini bado
wamekuwa wakiendelea kujitolea kusaidia kuimarisha ulinzi wa mataifa
mengine ambayo hali ya usalama inakuwa siyo ya uhakika.
“Tumefurahishwa
na historia ya Tanzania ya kuzisaidia nchi jirani kulinda amani na
kutatua migogoro ya hapo zamani na kuziwezesha kujipatia uhuru,” alisema
Manyama.
Aidha
Manyama alisema Umoja wa Mataifa umekuwa ukijitahidi kuendelea
kushirikiana na wanachama wake ili kwezesha upatikanaji wa amani kwa
mataifa yote na itaendelea kutoa heshima yake kwa wanawake na wanaume
ambao walipoteza maisha wakiwa kazini kulinda amani ya mataifa mengine.
“Mwaka
jana idadi ya waliokufa ilikuwa 129, walinda amani hawa walitoka katika
nchi 50, wakiwa ni pamoja na wanajeshi, polisi, watumishi kutoka
mataifa mbalimbali, wafanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa na
watumishi wa ndani,
“Tunapenda
kutoa heshima kwa mashujaa wetu zaidi wanaume na wanawake milioni moja
waliotumikia chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa kwa majivuno, weledi
tangu kuanza kwa kazi hiyo 1948,” alisema Manyama.
Nae
mgeni rasmi katika siku hiyo, Meja Jenerali James Mwakibolwa
aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa jinsi wanavyofanya kazi na kusaidia
kuokoa maisha ya watu wengi na kuahidi Tanzania itaendelea kutoa
wanajeshi wake ili waendelee kulinda amani.
“Tumeshatoa
walinda amani 2,328 katika operesheni mbalimbali zilizopita na
tutandelea kufanya kazi pamoja ili kuimarisha amani na utulivu katika
maeneo mengine,” alisema Meja Jenerali Mwakibolwa.
No comments:
Post a Comment