Mbali na hilo amesema atafuatilia na kuibua kero ambayo wanachi wa kata ya Msalato eneo la Kitelela ambao waliondoka katika maeneo yao kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege lakini hawajapewa fidia zao.
Mavunde alitoa kauli hiyo jana katika viwanja vya Bunge wakati wa kipindi cha zoezi usajili linaloendelea mjini hapa.
Mbunge huyo mteule alisema katika wilaya ya Dodoma kuna matatizo mengi likiwemo la migogoro ya ardhi.
Amesema matatizo ya ardhi kwa Dodoma ni kubwa na linatakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Akizungumzia juu ya wananchi ambao walipisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege mbune huyo alisema ni lazima wananchi hao walipwe fidia yao.
Amesema atapambana kwa kila jambo ili kuhakikisha wananchi hao wanapata fidia zao badala ya kuendelea kusumbuka.
Kwa upande wa Halmashauri alisema atashirikiana na viongozi pamoja na mkurugenzi kuhakikisha wanatafuta vyanzo vipya vya mapato.
“Lazima tuwe na ubunifu katika kutafuta vyanzo vipya mapato ambayo yataiwezesha Halmashauri kufanya miradi mingi ya maendeleo,” amesema Mavunde.
No comments:
Post a Comment