Mchakato wa kumwondoa Rais Dilma Rousseff wa Brazil
madarakani unaendelea baada ya kutokea mabishano kati ya viongozi wa
baraza la seneti na bunge la Congress ambao wamepinga maamuzi ya Kaimu
spika wa bunge.
Rais Dilma Rousseff wa Brazil
Kaimu spika wa bunge la Brazil Waldir Maranhao alibadilisha mchakato
wote kwa kusema unapaswa kuanza upya kwani ulikuwa na dosari.
Maranhao amesema mchakato wote ulikuwa na dosari kwani kura ya kwanza
ya bunge ilionekana kumhukumu Rousseff na kumnyima haki ya kujitetea.
Baraza la seneti limepinga maamuzi hayo na kusema linatarajiwa kupiga
kura katika kikao chake kitakachofanyika kesho (Jumatano) kuanzisha
mchakato wa kumfungulia mashtaka Rais Rousseff kwani lengo lao ni
kurekebisha maovu.
No comments:
Post a Comment