Manchester United moja ya timu vigogo wa ligi kuu ya England ambayo kabla ya ushindi wa sita mfululizo ilikuwa na wakati mgumu, sasa imeanza kupewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo maarufu duniani.
Manchester United Jumapili waliiangushia kipigo Liverpool kwa kuwacharaza magoli matatu kwa bila na kupanda hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 31 nyuma ya Chelsea vinara wenye pointi 39 na Manchester City wakiwa na pointi 36.
Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United, Phil Neville akizungumza na BBC Radio 5, alisema, Manchester United inaweza kutwaa taji la ligi hiyo.
"ndiyo wanaweza," amesema. "wachezaji wanaamini wanaweza kushinda taji hilo na ndivyo anavyoamini Louis van Gaal."
Neville, ambaye alishinda mataji sita ya ligi kuu ya England akiwa mchezaji wa timu ya Manchester United, na alikuwa sehemu ya timu ya makocha chini ya kocha mkuu David Moyes msimu uliopita ambapo ilikuwa na mwennendo mbaya.
United msimu huo ilimaliza katika nafasi ya saba, lakini Neville amesema moyo wa kitimu ulionyeshwa baada ya ushindi wa Jumatatu iliyopita dhidi ya Southampton hali inayomwaaminisha Van Gaal kushinda ubingwa.
No comments:
Post a Comment