TTCL

EQUITY

Wednesday, November 25, 2015

Daddy Owen kusaidia walemavu

Nyota wa muziki Daddy Owen wa nchini Kenya, ameweka nguvu zake katika kuendeleza shughuli za hisani hususan katika kusaidia walemavu katika jamii, akiwa amejipanga kushiriki katika matembezi ya watu wenye ulemavu huko Kenya, Desemba 3.

Nyota wa muziki Daddy Owen wa nchini Kenya akiwa na mke wake
Daddy Owen ambaye atafanya kazi hii akishirikiana na wadau wengine, wamepanga kufanya matembezi hayo katika siku hiyo ikiwa ni siku ya wenye ulemavu duniani, tukio hilo likiwa ni la kwanza na la aina yake kufanyika katika jiji la Nairobi.

Msanii huyo amejijengea heshima na kutambulika kwa mchango wake mkubwa wa kusaidia walemavu hususani wale wenye vipaji maalum, akiwa pia ni muasisi wa tuzo za Malaika ambazo hutambua pia mchango wa kundi hilo katika shughuli mbalimbali hususan sanaa kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment