TTCL

EQUITY

Wednesday, November 4, 2015

Dk. Magufuli atakiwa kufuata ya Mwl. Nyerere

Rais Mteule wa Tanzania, John Magufuli akiweka taji la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
Rais Mteule wa Tanzania, John Magufuli akiweka taji la maua katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere

SHIRIKISHO la Mchezo wa Bao Tanzania, (Shimbata) umemtaka Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuvaa viatu vya hayati Mwalimu Julius Nyerere kukuza na kuendeleza michezo ya jadi.

Rais wa Shimbata, Monday Likwepa wakati akitoa salam za pongezi kwa niabaya shirikisho, dhidi ushindi wa Dkt. Magufulina wa kuchaguliwa na wananchi kwa ushindi mnono, na kutangazwa kuwa rais mteule, amesema kuwa mchezo wa bao ni mchezo wa amani uliosaidia kuung’oa utawala wa kikoloni na kisultani ikiwa kama moja wapo ya kukutana na kupanga mikakati ya kupambana na ubeberu.

Likwepa amesema pamoja na Mwl. Nyerere kuwa na upenzi wa michezo yote pamoja na michezo ya jadi, yeye binafsi alikuwa anapenda mchezo wa bao.

“Hayati Mwalimu Nyerere alitoa vikombe na kuanzisha mashindano yaliyojulikana kama Operesheni futa madeni (Ofuma)” amesema Likwepa.

Aidha ujumbe wa shirikisho hilo umemtaka pia rais huyo mteule kurejea matamko na msisitizo wa Mwl. Nyerere katika kukuza na kudumisha utamaduni wa Taifa la Tanzania ikiwemo ile aliyosema katika moja ya mikutano yake kuwa “Taifa ambalo halina utamaduni wake ni sawa na nchi isiyokuwa na mwelekeo. Utamaduni nikioo na moyo wa Taifa lolote.”

No comments:

Post a Comment