Ushindi wa John
Pombe Magufuli wa CCM umetoa fursa kwa Bi Samia Suluhu Hassani kuhudumia
taifa hilo la Afrika Mashariki kama mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa
rais wa Tanzania.
Lakini Bi Samia ni nani?
Tangu kongamano
la Chama tawala nchini Tanzania CCM kumteua Daktari John Pombe Magufuli
Joseph kuwa mshika bendera wa CCM, Chama hicho kiliweka historia kwa
kumteua Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza.
Tangu Dodoma, Bi Samia aliwekwa kwenye ramani ya wanasiasa wanawake waliobobea barani Afrika.
Lakini Bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu ana umri wa miaka 54.
Kwa wale wanaomjua Bi Samia wanasema kuwa ni mchache wa maneno.
Asili yake ni Kisiwani Zanzibar.
Bi
Samia Suluhu Hassan amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika
serikali ya Muungano wa Tanzania na kadhalika amewahi kutumikia serikali
ya visiwani Zanzibar kama waziri katika afisi ya makamu wa rais.
Wakati wa kampeni za urais 2015 |
Ni mwanamke wa Kwanza kuwa Mgombea Mwenza
Tangazo la kumtaja kama mgombea mwenza wa rais
mteule wa tano wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania sasa limezaa matunda
na kumuweka Bi Samia katika mstari wa mbele barani Afrika kama naibu
rais wa Jamhuri ya Tanzania.
Chama CCM pia kimeingia katika daftari la vyama vilivyowapa wanawake sauti katika serikali yake katika karne hii ya 21.
Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976.
Masomo
Aliajiriwa
kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi, kazi
ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika
chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.
Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.
''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''
Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''
''Sio
rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya
siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.
Familia
Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .
Walijaliwa watoto wanne.
Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar.
Makamu wa Rais Mteule Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais Mteule wa Tanzania Mh. Dkt. Pombe Magufuli wakati wa kampeni za Urais |
Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.
Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.
Haikuchukua muda nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume.
Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri.
Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.
Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano.
Wadhifa aliohudumu hadi RAIS MTEULE Dkt John Pombe Magufuli alipomtangaza kuwa mgombea mwenza.
No comments:
Post a Comment