Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi
wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo
salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.
Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha
kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na
ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa” amesema Mwambene.
Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha
Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema
Mwmbene na kuongeza.
Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi
ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma
kupotoka.
Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya
uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo
wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.
No comments:
Post a Comment