TTCL

EQUITY

Wednesday, November 25, 2015

Wachezaji 36 kushiriki mashindano ya Chess TZ

Wachezaji zaidi ya 36 kutoka nchi zaidi ya sita wanatarajia kushiriki mashindano ya wazi ya kitaifa mchezo wa Chess yanayotarajiwa kufanyika Novemba 27 jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa Chess nchini TCA Nurdin Hassuji amesema, washiriki waliohakiki mpaka sasa ushiriki wa mashindano hayo ni kutoka nchini Afrika Kusini, Uganda, Rwanda, Kenya, India na Uingereza ambapo wanaamini mashindano hayo yatasaidia kuutangaza zaidi mchezo huo hapa nchini.

Hassuji amesema, wameshaanza kutoa mafunzo ya mchezo huo kwa baadhi ya shule za jijini Dar es salaam na wanatarajia kuukuza mchezo huo katika mashule mbalimbali hapa nchini li kuweza kupata vijana wengi watakaoweza kuutangaza mchezo huo kwa ndani na nje ya nchi.

Hasssuji amesema, mchezo huo unasaidia kukuza uelewa wa mwanafunzo hususani katika yale masomo yanayotakiwa kufikirika sana.

No comments:

Post a Comment