Kilimo ni uti wa mgongo wa nchi
yetu, lakini, baadhi ya wanasiasa, sio tu wamekipa mgongo, bali
wanakidhihaki tena hadharani. Baadhi ya kauli zao, hata za kuombea kura
ni zenye kuwakatisha tamaa hata vijana waliokuwa na ndoto za kushiriki
kilimo.
Kauli
zenye kurudiwarudiwa kama; " Wakulima wananyonywa" Ni nani anayetaka
kwenda kwa wanaonyonywa. Tungedhani wanasiasa hao wangesisitiza umuhimu
wa kilimo na kuwatia shime vijana wakiwamo wasomi, waende kwenye kilimo
ili wawe wengi na kupambana na huo unyonyaji.
Maggid.
Maggid.
No comments:
Post a Comment