pichana ni jopo la wapatanishi
Mashirika
manne yaliyopatanisha mzozo wa kisiasa nchini Tunisia yametunukiwa Tuzo
ya Amani ya Nobel ya mwaka huu kwa mchango wake katika kufanikisha
demokrasia nchini humo.
Akitangaza
mshindi wa tuzo hiyo kuu, mwenyekiti wa kamati ya Nobel amesema kuwa
kundi hilo la mashirika lilitoa mchango mkubwa katika kukuza demokrasia
baada ya maandamano ya mwaka 2011.
Mashirika
hayo manne ni muungano wa vyama vya wafanyakazi Tunisia (UGTT),
shirikisho la viwanda, biashara na kazi za mikono (UTICA), shirikisho la
watetezi wa haki za binadamu Tunisia (LTDH) na chama cha wanasheria
Tunisia.
Mashirika hayo manne yalikuwa miongoni mwa mashirika na watu 273 walioteuliwa kuwania tuzo hiyo.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Papa francis ni miongoni mwa watu mashuhuri waliopigiwa upatu kushinda.
''Mashirika
haya yanashirikisha sekta tofauti za maadili katika mashirika ya
kijamii Tunisia. Maisha ya ajira, maslahi, sheria na haki za
kibinaadamu," amesema mwenyekiti wa kamati hiyo ya Nobel Kaci Kullmann
Five.
waandamanaji wa Tunisia
Ni
kutokana na hilo ndiposa wanne hawa walichukua majukumu yao kama
wapatanishi ili kusukuma gurudumu la demokrasia na maendeleo nchini
Tunisia kwa ari na maadili ya hali ya juu.
Kundi
hilo lilitoa njia mbadala ya kuendeleza siasa kwa njia ya amani wakati
ambapo taifa hilo lilikuwa limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hatua yao
ilitoa fursa katika kuiwezesha Tunisia, katika kipindi cha miaka
michache, kuanzisha serikali ya kikatiba inayowapatia raia wake haki zao
za kibinadamu bila kufuata jinsia, siasa ama hata dini.
Amesema
kuwa kamati hiyo ya Nobel ina matumaini kwamba tuzo hiyo itachangia
katika kulinda demokrasia nchini Tunisia bali na kutoa msukumo kwa wale
ambao wanataka kuimarisha amani na demokrasia Mashariki ya Kati, Afrika
Kaskazini na dunia nzima kwa jumla.
Ushindi wa mashirika hayo ulipokelewa kwa shangwe na raia na viongozi nchini Tunisia.
No comments:
Post a Comment