Mgombea
Urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa Mhe. Edward Lowassa jana
jioni alikutana na wanawake wa Dar es Salaam kwenye Mkutano uliondaliwa
na Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) wakishirikiana na vyama wenza
katika Ukawa CUF, NCCR Mageuzi na NLD. Mkutano huo uliofanyika katika
ukumbi wa Millenium Tower ukiwa na kauli mbiu: "Lowassa na hatma ya changamoto za wanawake Tanzania"
Akizungumza
na wanawake hao Mama Regina Lowassa alielezea changamoto mbalimbali
zinazowakabili kina mama na Tanzania kwa ujumla zikiwemo sheria
kandamizi za mirathi na ndoa, mazingira magumu katika elimu, matumizi ya
nishati ya kuni na umaskini uliokithiri na mfumo wa dume. Aliwataka
kina mama hao kushirikiana kwa pamoja kufanya maamuzi sahihi ili kuweza
kuleta mabadiliko.
Nae
Mhe. Lowassa aliwashukuru wanawake wa Dar es Salaam kwa mahaba yao na
pia kumshukuru mwenyekiti wa Bawacha Bi. Halima Mdee kwa mualika,
Lowassa aliwataka wanawake hao kumuombea kura si tu kwa waume zao bali
kila mahali wamuombee kura.
No comments:
Post a Comment