WAKILI WA ZITTO ALBERT MSANDO.
Kwa marafiki zangu, Hatujashinda kesi dhidi
ya chama. Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA.
Natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya
CHADEMA mojawapo ya madhumuni ya chama ni kuendeleza na kudumisha Demokrasia
katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika
jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za
wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani
huru, wa haki na wa wazi ....
Pia natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya
chama Wajibu wa mwanachama wa Chadema ni kuwa tayari kupambana na namna yeyote
ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi.
Wajibu huu ni ndani na nje ya chama,Hatuwezi
kutekeleza wajibu upande mmoja.
Binafsi ninalo jukumu kutekeleza wajibu wangu
kwa manufaa ya chama,Kumekuwa na lawama, shutuma na malalamiko kwamba
nilichokifanya kinadhoofisha chama.
Napinga kwa nguvu zangu zote. Inawezekana
kabisa nilichofanya kinadhoofisha watu wachache ndani ya chama ila sio CHAMA.
CHADEMA sio mtu binafsi Ni taasisi Wanachama
wake ndio nguzo muhimu.
Sio Zitto wala Mbowe wala Slaa. Hawa ni
viongozi tu ambao wajibu wao ni kuendelea kujenga chama.
Uwezo wao upimwe kwa matokeo ya sasa. Sio kwa
mvuto na haiba zao. Fundisho la haya yote ni moja: KUVUMILIANA SIO KUFICHIANA
SIRI AU UDHAIFU.
Kosa limetendeka na kukubali kosa sio dhambi Ni
wazi kabisa kumekuwa na kutokuelewana kwa muda mrefu.
Ni dhahiri viongozi wetu wamekuwa wanajua
udhaifu wa kila mmoja wao.
Lakini kwa sababu ambazo hazijawa wazi
waliamua kukaa kimya. Au labda ilikuwa ni kwa kuamini kwamba yatamalizika bila
athari.
Sasa matokeo yake ndio haya. Kinachohitajika
sasa sio kutafuta mchawi.
Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwajibika
ipasavyo na kuhakikisha suluhu inapatikana.
Na niseme wazi kabisa, kama suluhu ni mtu
kufukuzwa basi tuhakikishe hilo linafanyika kwa mujibu wa Katiba na Kanuni kwa
kuzingatia haki za msingi kama ambavyo tumekuwa tukipigania.
Haki itendeke, na zaidi lazima ionekane
imetendeka,Pamoja tunaweza.
Mwisho, tusiruhusu muendelezo wa 'ufuasi' wa
watu ndani ya chama.
Tuwe wafuasi wa misingi ya chama. Bado nafasi
ipo ya kurekebisha pale tulipoangukia kama busara na hekima vitatumika.
Nawatakia kila kheri ndugu zangu.
"In
a battle for the minority rights we have to promote the rights of the majority
and we will remain united" AGM 2014.
No comments:
Post a Comment