Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),
Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa
Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam
jana.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya
Ukimwi, Hassna Sudi Katunda Mwilima (wa pili kulia), akifafanua jambo
kwa wajumbe hao na wageni katika ziara hiyo.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (kulia), akiwatembeza wajumbe hao MSD Keko.
Meneja wa Miradi Msonge, Byekwaso Tabura (katikati), akitoa maelekezo kwa wajumbe hao.
Na Mwandishi Wetu
WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
masuala ya UKIMWI na dawa za kulevya wametembelea Makao makuu ya Bohari
ya dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam. Katika ziara yao kamati
imeishauri serikali kutenga bajeti ya dawa na vifaa tiba kulingana na
mahitaji.
Akitoa ufafanuzi kuhusu asilimia 80% ya
dawa kuagizwa nje ya nchi, Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu
amesema bado hakuna viwanda vya ndani vya kutengeneza dawa ,na vichache
vilivyopo havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya MSD.
Katika hatua nyingine,wajumbe wa kamati
hiyo ya Bunge ya masuala ya UKIMWI,inayoongozwa na Mhe.Hassna Sudi
Katunda Mwilima(Mb.) imeipongeza MSD kwa kuwa na maghala ya kisasa ya
kuhifadhia dawa,huku wakihimiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto ishughulikie deni la serikali. Aidha, walisema
kulipwa kwa deni kutasaidia MSD kununua dawa muhimu kwa wakati.
Kuhusu deni, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya
alieleza kuwa suala la deni linafanyiwa kazi.
Hata hivyo Naibu Waziri Dkt. Hamisi
Kigwangalla amethibitisha kuwa tayari serikali imeshaahidi kupunguza
deni kwa awamu kuanzia mwaka huu wa fedha.
No comments:
Post a Comment