HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI LOWASSA YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU
Baada ya miaka ishirini na tano tangu mfumo
wa vyama vingi urejeshwe, vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na
NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi kupigania uchaguzi
mkuu wa mwaka huu na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za CCM na waasisi wake,
umekuwa utawala wa wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama elimu, afya, maji na makazi.
Mabadiliko ya kuondoa umaskini.

Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili hali zao za maisha.
Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa pato laTaifa linakuwa.
Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na barabara bora zinajengwa.
Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa. Wanataka makazi bora.
CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na ujinga inahitimishwa.
Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya fikra, uongozi, sera na utendaji.
Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera hizi.

Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha ya wananchi.
Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma. Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji safi.Ndugu watanzania
CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa mikakati sahihi na siyo nadharia.
Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao leta maendeleo.
Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa umaskini utakuwa na nguzo tano:-
Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio halisia kutoka wawekezaji
Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya, maji na makazi, na mazingira
Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo. Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu na pia:-
Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika soko la ajira.
Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na shule za Kata.

Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote nchini.
Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za wanafunzi.
Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia, usafiri na zana za teknolojia.
Kufuta michango ya maabara ya shule za kata
AFYA
Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi ya jamii

Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga kupunguza gharama za tiba.
Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili kuleta tija na huduma stahiki.
Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na kujenga hospitali za kisasa
ili kusogeza huduma za afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za
nje ya nchi.
Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na nyumba na usafiri.
Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za afya bila kuathiri
uendeshaji wa watoaji huduma za afya kama vile serikali na hospitali za
sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
ARDHI, MAJI NA KILIMO
Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa Watanzania na kudhibiti migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
Tutapima ardhi yote ya Tanzania na kumilikisha vijiji na wakulima kwa hati za serikali ili kuipa thamani.
Tutaleta mapinduzi ya kilimo kwa kuimarisha elimu, ufundi na teknolojia
ya kisasa na kumkomboa mkulima kutoka jembe la mkono.
Tutasimamia kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa na kuunganisha sekta hizo na ya viwanda.
Kuhakikisha kuwa wananchi wanatunza na kulinda vyanzo vya maji.
Tutakuza kilimo cha umwagiliaji kwa kuwapa wakulima elimu na mikopo ya
riba nafuu ya kuvuna maji na kujenga miundombinu husika.
Tutaweka
mazingira rafiki yatakayomhakikishia kwa kila Mtanzania kupata maji
safi na salama. Kumaliza kero za maji nchini kutamkomboa mwanamke
kutokana na adha ya kuchota maji kwa kichwa.
Nitafuta kodi zote za mazao na mifugo kwa wakulima na wafugaji.
Tutasimamia kilimo cha biashara kinachozingatia maslahi ya nchi na ya Watanzania.
Tutaanzisha programu maalum ya kufufua mazao asilia ya Tanzania hususan mkonge.
Tutaanzisha Benki ya Maendelo ya Ufugaji na Uvuvi.
MIUNDOMBINU
Tutaboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.

Tutajenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
Tutajenga reli ya kati kwa viwango vya kisasa
Tutajenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
Tutajenga miundombinu ya kisasa na kuondosha misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha
Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini ili kufikia zaidi ya asili mia sabini na tano ya Watanzania
VIWANDA
Tutaimarisha sekta ya viwanda kuwa mhimili wa uchumi kwa uzalishaji wa bidhaa na ajira endelevu.
Tutajenga viwanda vipya vya kusindika mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.
Tutahakikisha kuwa ndani ya miaka mitano mali ghafi zote za Tanzania zinasindikwa kabla ya kusafirishwa nje ili kuongeza mapato na ajira ya mamilioni ya vijana.
Tutaanzisha Benki ya Ukuzaji wa Viwanda
UCHUMI

Tutabadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi
wa Tanzania unakuwa ni wa soko-kijamii ambapo nguvu za soko zitatumikia
jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za
kijamii zinapatikana kwa ufanisi.
Tutalinda sekta binafsi na
bidhaa za ndani kwa kuwapa Watanzania upendeleo wa maksudi kwa kipindi
cha mpito ili waimarike na waweze kuhimili ushindani. Tutawapa
wafanyabiashara wetu upendeleo katika manunuzi ya serikali na kuwajengea
mazingira mazuri ya biashara na kodi endelevu.
Tutawawezesha Watanzania kupata mitaji ya biashara kwa masharti nafuu kabisa.
Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
Tutavutia uwekezaji na wawekezaji wenye tija. Kuweka udhibiti wa wahamiaji wasioleta tija wala maslahi kwa Taifa.
Tutaimarisha sera ya ubia baina ya Serikali na Sekta binafsi kwenye
maeneo muhimu ya kiuchumi na kibiashara. Pia, kuwawezesha Watanzania
kuwekeza kwa njia ya ubia na wawekezaji wenye mitaji mikubwa bila kujali
wanapotoka.
Tutaimarisha usimamizi kwa kubadilisha mfumo wa
Vyama vya Ushirika nchini ili utokane na uendeshwe na wakulima wenyewe
ikiwa na pamoja na kuwawezesha kuboresha makazi kwa mpango wa
kushirikiana kujenga nyumba bora.
Tutaanzisha na kuwezesha
uanzishaji wa viwanda vidogovidogo vinavyotoa ajira kwa wingi kwa
kuvihusisha na vyuo vya ufundi na benki maalum kwa lengo hilo.
AJIRA
Tutasimamia swala la ajira hasa kwa vijana kwa kukuza elimu ya ufundi ili waweze kujiajiri.
Tutazipa kipaumbele sekta zinazozalisha ajira kwa wingi hasa za viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na utalii na kuzipa unafuu wa kodi ili zikue kwa haraka.
Tutawapa wawekezaji wakubwa katika sekta hizi upendeleo maalum na viwango vya kodi nafuu.
NISHATI NA MADINI
Serikali itashiriki kikamilifu katika uzalishaji wa nishati.
Itatengeneza mazingara mazuri ya kisera yatakayovutia na kuwezesha ushiriki wa Watanzania na ubia kati yao na wageni.

Serikali yangu itaupa uzalishaji mkubwa wa umeme wa maji kipaumbele
namba moja, umeme wa makaa ya mawe kipaumbele namba mbili, umeme wa gesi
asilia kipaumbele namba tatu na umeme wa urana kipaumbele namba nne.
Serikali itatoa vipaumbele muhimu kwenye usambazaji wa huduma kubwa ya
umeme sehemu za uzalishaji uliyolenga masoko ya ndani, ya nchi jirani na
ya nchi za kigeni.
Itapitia upya mikataba yote mikubwa ya nishati na madini ili kubaini iliyo mibovu na kuifanyia maboresho.
Serikali yangu itatumia sehemu ya hisa zake kwenye raslimali kubwa ya
gesi asilia iliyopatikana hapa nchini kama rehani kwenye kujichukulia
mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya mabomba ya gesi.
Serikali itatoza kodi na ada ndogo zaidi kwa wazawa wenye ubia kati yao
na wageni kuliko zitakazotozwa kwa wageni wasiowekeza kwa kushirikisha
wazawa.
Serikali itasitisha utoaji wa misamaha ya kodi isiyo
lazima kwenye sekta ya madini, na badala yake itawekeza kwenye kuongeza
thamani ya raslimali zake za madini.
Tutakuza nishati mbadala kutamkomboa mwanamke kutokana na adha ya kukata kuni
MALIASILI NA UTALII
Tutasimamia uvunaji na matumizi ya rasilimali za Taifa kwa manufaa ya kila Mtanzania wa kizazi hiki na kijacho.

Tutapiga vita ujangiri na kuimarisha utunzanji wa hifadhi za taifa na mazingira.
Tutachochea ujenzi wa miundombinu ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mahoteli na kuimarisha mafunzo
Tutaongeza idadi ya watalii kufikia milion mbili ifikapo 2020
UTAWALA BORA, ULINZI WA NCHI NA USALAMA WA RAIA
Tutasimamia Katiba mpya inayolinda haki za msingi za wananchi na kuweka bayana mipaka ya madaraka ya serikali na viongozi, Bunge na Mahakama.
Tutaboresha miundobinu ya sheria na kuimarisha utendaji wa Mahakama na maslahi ya wafanyakazi
Tutasimamia haki za raia na kuangalia upya sheria kandamizi ili wananchi kama Masheik wa Zanzibar hawasoti jela kwa sababu za kisiasa.
Tutaimarisha mafunzo ya vyombo ya Polisi hasa wapelelezi na waongoza mashtaka ili wapate uwezo wa kusimamia utoaji wa haki.
Tutavipa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nyenzo na kuboresha mazingira yao ya kazi na maslahi
UZALENDO, UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI

Tutajenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini mchango wake kwa taifa kila siku
Tutaimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika Sekta ya Umma
Tutaimarisha mchango wa Wataalam wetu, wanawake na vijana katika
kusimamia uchumi na kuwajengea mazingira stahiki ya kazi pamoja na
mafao.
Tutapiga vita rushwa na ubadhirifu katika sekta ya Umma na binafsi
Tutadhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na kufuta
safari za watumishi serikalini zisizokuwa muhimu pamoja na zile za Rais
na kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini.
Tutadhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
Tutaimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za serikali na
kuweka bayana mikataba yote ya nchi ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta,
madini na gesi asilia
KUKUZA PATO LA SERIKALI
KUKUZA PATO LA SERIKALI
Tutadhibiti mapato kutokana na raslimali kwa kupitia upya viwango vya
mirabaha kutokana na madini na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa Tanzania
inapata gawio stahiki.
Serikali itaanzisha Wizara maalum itakayosimamia nishati ya gesi na mafuta.
Tutaimarisha ofisi ya Msajili wa Hazina ili kusimamia vema uwekezaji wa Serikali katika mashirika na mapato yake.
Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yanaendeshwa kwa misingi ya faida na uadilifu.
Tutadhibiti ukwepaji kodi za ushuru wa forodha na kupiga marufuku
misamaha ya kodi holela ili kuokoa mabilioni ya fedha yanayopotea kila
wiki.
Sambamba na hilo tutarahisisha utaratibu wa kulipa kodi ili
kuondoa kero na mazingira ya rushwa. Kwa kudhibiti makusanyo ya kodi
tutakusanya fedha za kugharimia huduma za msingi kama afya na elimu
kikamilifu.
KUIMARISHA MUUNGANO
KUIMARISHA MUUNGANO
Tutaimarisha umoja, usalama na udugu wa Watanzania na Muungano kwa misingi ya haki na usawa
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
WANAWAKE, WATOTO NA WAZEE
Wanawake watapewa fursa na haki sawa katika elimu na uchumi ili waweze bila kuwezeshwa.
Tutahakikisha wazazi wanapata fursa ya kuwa walezi na wafanyakazi kwa kuongeza urefu wa likizo ya uzazi
Tutaimarisha elimu ya watoto hasa wasichana na kukuza fursa zao na kukomesha ndoa za watoto wadogo.
Tutaongeza uwakilishi wa akina mama katika ngazi zote serikalini na mashirika yake kufikia asili mia hamsini ifikapo 2020.
Wazee na wasiojiweza watapewa posho ya kujikimu inayokidhi mahitaji ya
msingi itakayowawezesha kuishi kwa heshima na kulinda utu wao ndani ya
familia na jamii zao.
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
SANAA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo
Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa
Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.
Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia
Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani
ya miaka mitano
Tanzania inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya
kimataifa ya soka na riadha
Tutalinda Hakimiliki za sanaa nchini
7. Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.
SERA YA MAMBO YA NJE YENYE TIJA KWA TAIFA
Tutakuza ushirikiano wa Kimataifa wenye tija na Ujirani mwema.
Tutatetea haki za binadamu, usawa wa nchi na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
Tutakuza umoja na ushirikiano wa Umoja wa Afrika, Jumuia ya Afrika Mashariki, SADC na Umoja wa Mataifa.
Tutaimarisha Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kudai mabadiliko ya mfumo ili kuleta usawa wa nchi shiriki.
Ndugu Watanzania, naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
Ndugu Watanzania, naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo
Natambua kuwa uongozi ni dhamana. Mkinichagua nitaienzi dhamana hiyo kwa utendaji uliotukuka.
Nawaahidi Watanzania kuwa kwa uwezo, akili, uzoefu na nguvu zangu zote
nitawatumikia. Nawaomba nanyi mniahidi jasho lenu na uwezo wenu wote ili
kwa pamoja tuvuke. Tutajikomboa toka utawala wa CCM unaodumaza uchumi
na maendeleo. Tutaanza safari ya uhakika kuondoa umaskini.
Mabadiliko pia ni kuthamini utu na kukataa hadaa ya hongo ili kuuza haki
yako ya kuchagua. Msikubali rubuni za uchaguzi kwa kupewa pesa au vitu.
Rushwa ya uchaguzi ndiyo sera ya CCM. Ukikubali basi umeuza pia haki na
sauti yako ya kuwalalamikia walio madarakani. Imetosha. Tukatae.
Tulinde utu na haki zetu. Tuchague mabadiliko.
Mabadiliko ni
fikra. Ni kufikiri na kutenda tofauti. Hatuwezi kuendelea kufikiri na
kutenda kama kwamba hatuna dharura ya maendeleo. Kwanza tuanze kwa
kufanya mabadiliko na tujiamini kuwa sisi kama Taifa tunaweza. Tunaweza
kujitegemea na kuleta maendeleo yetu wenyewe bila kutegemea wafadhili.
Hii si ndoto. Nchi nyingi zimefanikiwa kuondoa umaskini katika kizazi
kimoja. Tujifunze kutoka kwao.
Tuwe taifa linalotumia raslimali
zake kujiendeleza na siyo kuwanufaisha wageni na kuwafanya Watanzania
watwana katika nchi yao. Inabidi tuache kuwa taifa ombaomba. Tuache
kuukubali na kuvaa umaskini kama joho la fahari.
Mabadiliko ya
kweli hayawezi kuletwa na CCM. Tusitegemee kuwa leo wana jipya. Ndiyo
maana ahadi walizotoa miaka thelathini iliyopita ndizo wametoa juzi.
Tukatae hadaa. Miaka hamsini ya CCM imetosha.
Tunaamani kwamba
tutashinda kwa sababu Watanzania mpo nyuma yetu. Watanzania mmeamua
kuleta mabadiliko. Kura yako ndiyo itakayokuwa mkombozi wako. Hakikisha
unapiga na kuilinda kura yako. Wakati wa mabadiliko ni sasa.
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni san
Mungu ibariki Tanzania. Asanteni san
No comments:
Post a Comment