Vijana wametakiwa kugeuza changamoto kuwa fursa na kuwa na utamaduni wa kujiajiri na kuchapakazi kwa bidii badala ya kusubiria kuajiriwa huku wakilaumu mamlaka zinazoshughulika na vijana nchini.
Hayo yamesemwana Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua mdahalo wa siku mbili kujadili hatma ya ajira kwa vijana Tanzania uliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) jana jijjni Dar es Salaam.
“Changamoto ya ukosefu wa ajira inaweza kutumika kama fursa kwa kijana anayejitambua kwakuwa na fikra chanya itakayomuwezesha kutumia elimu aliyoipata kujiajiri bila kuona aibu kufanya baadhi ya kazi mbali ya kuwa amesoma hadi elimu ya juu hivyo kujiongezea kipato,”alisema Prof. Gabriel.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bi. Mary Kawar amesema kuwa shirika hilo liko tayari kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya ajira ili kupunguza tatizo la ukosefuwaajira kwa vijana.
Naye mshiriki wa mdahalo huo Bw. Masson Kimbo ameiomba serikali kupitia mifumo ya elimu nchini itakayowawezesha vijana kujengewa uwezo wa kujiajiri na kuwa na fikra pana katika masuala ya ujasiriamali.