TTCL

EQUITY

Thursday, February 18, 2016

Upigaji kura wachelewa maeneo mengi Uganda

(Mitandao ya kijamii) Facebook, Whassap zazimwa Uchaguzi wa Uganda

Mitandao ya kijamii imezimwa hii leo nchini Uganda wakati wa zoezi muhimu la kuchagua Rais pamoja na wabunge wa kuwawakilisha wananchi.

Rais wa nchi hiyo Yoweri Musevrni amenukuliwa akisema kuwa mitandao hoyo imezimwa kwa lengo jema la kuzuia kusambaza taarifa za uongo na za kichochezi ambazo zinaweza kusababisha matatizo katika taifa hilo.
Kituo kimoja cha uchaguzi uchaguzi wake umesitishwa jijini Kampala baada ya kutokea kutoelewana baina ya wananchi na askari waliokuwa wakilinda amani na usalama.
Aidha Mgombea Urais Dkt. Kiza Besgye amesema haamini kama uchaguzi huo utakuwa huru na haki kuanzia upigaji kura hadi upatikanaji wa matokeo.

 
Upigaji kura unafaa kuanza saa moja asubuhi kwa mujibu wa sheria 
 
Mjini Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo, tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo. Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo muda wa kupiga kura ungeongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii ilisema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.

Uchaguzi
Mwangalizi mkuu wa Jumuiya ya Madola Olusegun Obasanjo (kushoto) akizungumza na baadhi ya wapiga kura Kampala 
 
Raia katika maeneo mengi nchini humo pia wamelalamikia kutatizika wakiingia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Facebook na WhatsApp, kwa kutumia simu. Serikali haijaeleleza ni nini chanzo cha matatizo hayo.
Kuna wagombea saba wa urais wanaojaribu kuhitimisha uongozi wa Rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 30 sasa.

Wanaotoa ushindani mkubwa kwa Bw Museveni ni mgombea wa FDC Kizza Besigye na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.
Kuna jumla ya wapiga kura 15 milioni ambao wamejisajili kupiga kura nchini humo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.

No comments:

Post a Comment