Spika wa Bunge JOB NDUGAI ameteua wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge ambayo inaundwa na wabunge 15
Spika wa Bunge Job Ndugai
Spika wa Bunge JOB NDUGAI ameteua wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge ambayo inaundwa na wabunge 15.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge jijini Dar Es Salaam imesema
kamati hiyo inatakiwa kufanyia marekebisho ya nyongeza ya NANE ya kanuni
za kudumu za bunge, kuhusu majukumu ya kamati zingine za bunge ili
kuendana na majukumu ya serikali kwa kuzingatia muundo wa Baraza la
Mawaziri.
Kamati hiyo inaundwa na Spika wa Bunge ambaye anakuwa mwenyekiti na
makamu wake ni Naibu Spika, huku Kiongozi wa Upinzani na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali wakiwa wajumbe kwa nyadhifa zao.
Wajumbe wengine walioteliwa na Spika ni MAKAME KASSIM MAKAME, TUNDU
LISSU, JASSON RWEIKIZA, ALLY SALEH ALLY, MAGDALENA SAKAYA, SALOME
MAKAMBA, Dkt. JASMINE BUNGA, ZAINAB KATIMBA, Balozi ADADI RAJAB, Dkt.
CHARLES TIZEBA na KANGI LUGOLA.
Wajumbe hao wanatakiwa kukutana tarehe 15 mwezi huu jijini Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo imesema Spika atakamilisha uteuzi wa Wajumbe katika
Kamati zingine za Bunge kabla ya kuanza kwa mkutano wa pili wa Bunge
unaotarajiwa kuanza tarehe 26 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment