TTCL

EQUITY

Saturday, March 19, 2016

WATOTO HUPATA MIMBA KIPINDI CHA LIKIZO

Na Ferdinand Shayo Arusha.
AfisaMaendeleo ya jamii  Mkoa wa  Arusha Blandina Nkini amesema kuwa watoto wengi hupata mimba kipindi cha likizo za mashuleni kutokana na ufuatiliaji mdogo wa wazazi kwa watoto wawapo mashuleni na majumbani hali inayochangia ongezeko la mimba za utotoni na kuzorotesha elimu.
 
Blandina alisema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa wazazi wengi hawana muda wa kukaa na watoto  wao kuzungumza na wanao juu ya maadili pindi wanaporejea kutoka shule za bweni.

Afisa huyo akizungumza katika mkutano wa kujadili mipango ya mwaka 2016 /17 ya shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tommorrow linalojihusisha na masuala ya watoto ,amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto hasa kipindi ambacho wanakua likizo ili kuwajengea uwezo juu ya changamoto  za ukuaji zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hilo Melisa Queyquep amesema kuwa kwa sasa wana mpango wa  kutoa mafunzo kwa kwa walimu 500 kwa miaka 5 .
Melisa alisema kuwa wameanzisha mpango huo mahususi  ili kuwezesha upatikanaji wa walimu bora kwani vigumu kuwa na elimu bora bila kuwa na walimu bora.
“Kwa sasa tunasomesha watoto 114  wanaosoma kwa ufadhili kwa kipindi cha mwaka  huu na pia wanatarajia kuwafikia watoto wengi wa kitanzania ambao ni yatima na wanaishi katika mazingira magumu” Melisa
Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo  aliyemaliza muda wake Arusha Kennedy Oulu alisema kuwa serikali inapaswa kuboresha elimu mbali na kujenga majengo  pia madawati,vyoo na vifaa vya kufundishia vitiliwe mkazo.

No comments:

Post a Comment