TTCL

EQUITY

Thursday, February 18, 2016

KIWANGO CHA UFAULU KIDATO CHA NNE 2015 CHA SHUKA KWA ASILIMIA 71.09

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha 4 ufaulu washuka

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la TANZANIA –NECTA, Dkt. CHARLES MSONDE amesema wasichana waliofaulu ni laki moja thelathini na moja 913 sawa na asilimia 64.84 wakati wavulana waliofaulu ni laki moja arobaini na moja elfu na 34 sawa na asilimia 71.09
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la TANZANIA –NECTA, Dkt. Charles Msonde.

Dkt. MSONDE amesema kiwango cha juu cha ufaulu ni kwa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 ya watahiniwa wamefaulu huku kiwango cha chini cha ufaulu kikiwa ni somo la Hisabati ambapo asilimia 16.76 wamefaulu mtihani huo.

Dkt. MSONDE amesema baraza la mitihani la TANZANIA limeamua kurejesha mfumo wa madaraja kufuatia maoni ya wadau yaliyoonyesha kuwa wengi wao hawana uelewa kuhusu mfumo wa viwango.

Katika matokeo hayo shule kumi bora ni KAIZIREGE mkoani KAGERA, Shule ya sekondari ya wasichana ya ALLIANCE, mkoani MWANZA, Shule ya sekondari ya wasichana na Saint FRANCIS, MBEYA, Shule ya sekondari ya wavulana ya ALLIANCE, MWANZA, Shule ya sekondari ya wasichana ya CANOSSA, DSM,Shule ya sekondari ya wavulana ya MARIAN, PWANI, shule ya sekondari ALLIANC ROCK ARMY mkoani MWANZA,Shule ya sekondari ya wasichana ya FEZA, jijini DSM, shule ya sekondari ya wavulana FEZA ya jijini DSM na URU SEMINARY iliyoko mkoani KILIMANJARO.

No comments:

Post a Comment