TTCL

EQUITY

Thursday, February 18, 2016

Wachina 13 wakamatwa mgodini Geita bila kibali

Idara ya uhamiaji mkoani Geita inawashikilia raia 13 wa China kwa tuhuma za kufanya kazi za kutafiti pamoja na kufanya kazi za kuchenjua madini ya dhahabu kinyume cha sheria.
 
Baadhi ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria 
 
Watuhumiwa hao wamekamatwa katika machimbo ya Igo katika kijiji cha Nyamahuna wilayani Geita kufuatia msako mkali kwa wageni wa mataifa kutoka nje wanaofanya kazi mkoani humo bila ya kuwa na kibali.
Akizungumza mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao afisa uhamiaji mkoa huo Charles Washima amesema watuhumiwa hao waliingia nchini kwa kibali cha matembezi lakini wamekuwa wakijihusisha na ufanyaji kazi kinyume na sheria.
Naye mmiliki wa mgodi huo Bi. Rehema Abdallah alishikiliwa na Idara hiyo baada ya kuhusika na kuwaleta raia hao wachina kufanya kazi katika mgodi wake bila ya kuwa na kibali maalum

No comments:

Post a Comment