Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
Tamko
hilo limetolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage baada ya kutembelea na kukagua viwanda vya serikali
vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji mkoani Morogoro.
Waziri Mwijage amemwagiza Mkurugenzi wa Viwanda wa wizara hiyo
kufuatilia wizara ya fedha na mipango, taratibu mbalimbali za kisheria
kwa wamilki wa viwanda vilivyofungwa ama kushindwa kuendeleza uzalishaji
kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.
Aidha Mwijage amesema lengo la serikali ni kuona viwanda vyote
vilivyobinafsishwa na kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa
vinafanya kazi za uzalishaji kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya
mikataba ili kuwawezesha kutoa ajira nyingi kwa watanzania.
No comments:
Post a Comment