TTCL

EQUITY

Tuesday, May 10, 2016

Mambo mengine ukisikia ni kama ndoto vile-Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amesema kuwa kuna mambo mengine ukiyasikia ni kama ndoto vile, kauli aliyoitoa baada ya kusikia kuwa Jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam, kuwa halina Zahanati.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Job Ndugai amesema mambo mengine ukisikia ni kama ndoto au hadithi za kufikirika, baada ya kusikia, Kata ya Vingunguti na Kipawa Jijini Dar es Salaam hazina Zahanati.
Hayo yamebanishwa na Wabunge wa Jimbo la Segerea, Mhe Bona Kalua pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia (CHADEMA), Anatropia Theonest katika maswali yao kwa Wizara ya TAMISEMI, ya kutaka kujua kwanini maeneo hayo yenye mkusanyiko wa watu hayana Zahanati.
Mhe. Bona Kalua alizitaja Kata ambazo hazina Zahanati katika jimbo lake ni pamoja na Kata ya Vingunguti ambayo inawakazi wengi na haina Zahanati lakini pia , Kata ya Kipawa, Minazi Mirefu, Kiwalani, Kisukulu na Kimanga zote hazina Zahanati wala Vituo vya Afya.
Katika majibu yake Naibu Waziri wa TAMISEMI ,Suleiman Jaffo, alikiri kuwepo changamoto hiyo katika jimbo hilo na kusema kuwa serikali inalifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kutafuta eneo kubwa ambalo litafaa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati pamoja na Vituo vya afya ili kuondoa tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment