TTCL

EQUITY

Monday, January 25, 2016

50 wafariki kwa baridi kali Taiwan

Watu 50 wamepoteza maisha kutokana na baridi kali nchini Taiwan ,baridi ambayo imeathiri pia upande wa Asia mashariki.


Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini Taiwan vinasema vifo hivyo vimetokana na kushuka sana kwa kiwango cha joto mwilini na wengine wakafariki kutokana na maradhi ya moyo.
Katika baadhi ya maeneo ya Taiwan, viwango vya joto vimeshuka hadi nyuzi 4C (39F) siku ya Jumapili.

Pia watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na baridi hiyo na uwanja wa ndege Jeju nchini Korea Kusini, umefungwa kwa kutokana na theluji.
Chanzo BBC.

No comments:

Post a Comment