Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, David Kafulila ameshindwa kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Husna Mwilima (CCM) iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora.
Kafulia ambaye alifungua kesi hiyo mwaka jana baada ya kushindwa katika nafasi ya ubunge na Husna Mwilima, kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Ferninand Wambari ambaye ameamua kuifuta baada ya kutokuwepo kwa uthibitisho wa kutosha.
Katika kesi hiyo ambayo Kafulila aliwakilishwa na mawakili watatu, Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera na upande wa Husna Mwilima aliwakilishwa na wakili Kennedy Fungamtama na Mawakili wa serikali ambao walimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.