TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Wakulima 300 wilayani Muheza wameigomea serikali kutoka katika mashamba yao.

Wakulima zaidi ya 300 waliopo katika vijiji vya Kibanda, Semngano na Mkinga wilayani Muheza wamekataa kuondoka katika mashamba yao yenye mazao ya kudumu kufuatia watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kwenda kuyapima na kuweka mawe ya mipaka kisha kuwaamuru kuachia mashamba hayo kabla nguvu ya dola haijatumika dhidi yao.

Wakizungumza katika mashamba hayo, baadhi ya wakulima wameiomba serikali kuharakisha kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo ya wakazi wa Muheza inayosababishwa na baadhi ya watumishi wake hatua ambayo imechangia sehemu kubwa ya wanacnhi kuichukia serikali yao kwa sababu ya watu wachache.
Wakifafanua jinsi walivyopata mashamba hayo baadhi ya wakulima wakiwemo wazee wamesema wameanza kulima tangu mwaka 1983 chini ya operesheni nguvu kazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa kwanza hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere la kuwataka wapande mazao ya kudumu ili waweze kujitosheleza kwa chakula.
Kufuatia hatua hiyo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Bwana Adrian Jungu akielezea sakata hilo amesema awali shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 454 lilikuwa likimiliwa na mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia lakini baadae halmashauri walilitaifisha shamba hilo baada ya mwekezaji kuondoka nchini.

No comments:

Post a Comment