
Jeshi
la Polisi kikosi cha usalama barabarani linawashilikia makondakta na
mawakala wa mabasi mbalimbali yanayofanya safari zake mikoani kwa kosa
la kuuza tiketi za kusafiria kwa bei ya juu kinyume na sheria ambapo
wakati hao wakiwa wanashikiliwa maelfu ya abiria wameshindwa kusafiri
kutokana na kutokuwepo kwa mabasi ya kutosha.
ITV imefika kituo cha mabasi Ubungo na kushuhudia idadi kubwa ya
abiria wakiwa hawajui nini cha kufanya kutoka na kukosa usafiri ambapo
wengine wamelazimika kusitisha safari zao na wegine wakidai kuwa
wamiliki wa mabasi wamebadilisha safari za mabasi yao ndio maana usafiri
umekuwa mgumu.
Akijibu tuhuma hizo msemaji wa chama cha wamiliki wa mabasi TABOA
Bw Mustaph Mwalongo amesema siyo kweli kuwa mabasi yamebadilisha safari
bali magari mengi yameenda mikoani na yanashindwa kurudi kwa sababu
hakuna abiria wengi wanaokuja Dar es Salaam.
Wakati hali hiyo ikitokea mkuu wa kikosi cha usalama barabarani
kamanda Mohamedi Mpinga amesema wapo watu ambao wanashikiliwa kwa
mahojiano zaidi kwa kosa la kuuza tiketi kwa bei ya ulanguzi na
watachukuliwa hatua za kisheria muda wowote uchunguzi ukishakamila.
Aidha ITV ikiwa kituoni hapo kilishudia kondakta wa basi la Abood
lenye namba za usajili T 517 AGD linalofanya safari zake kati ya Dar na
Iringa akiwa mikononi mwa polisi kwa kosa la kuuza tiketi kwa bei ya
juu.
No comments:
Post a Comment