
Ikiwa
ni katika kuunga mkono jitihada za serikali za kutoa elimu bure baadhi
ya wanachi ambao ni wazawa wameunga mkono mpango huo kwa kutoa madawati
milioni moja na nusu bure kwa shule ambazo zitakuwa hazina madawati
hatua ambayo itaipunguzia serikali gharama za kununua madawati na fedha
hizo kuelekezwa katika mambo mengine yanayohusu elimu.
Wakizungumza jijini Dar es Saalam baadhia ya watu waliojitolea
kutoa madawati wamesema wameguswa na jihada nzuri zinazofanywa na rais
Dk John Magufuli za kuinua kiwango cha elimu bure na hivyo wanaona ni
busara kuunganisha nguvu.
Naye bw oscar kaduma amesema kupitia rasilimali za mbao zilizopo
nchini wameona ni vyema wakatumia rasilimali hizo kuutengneza madawati
amabyo yatawasaidia wanachi wa kawaida amabo kwa miaka mingi sana
wamekuwa wakipata shida kwa watoto wao kukaa chini.
Hatua hiyo imeungwa mkono na baadhi ya wazazi na wanaharakati wa
elimu nchini na ambapo wamesema watoto wamekuwa wakikaa chini kwa muda
mrefu hatua ambayo ilikuwa inawafanya washindwe kufanya vizuri katika
masomo yao.
No comments:
Post a Comment