TTCL

EQUITY

Thursday, December 24, 2015

Soka ufukweni Zanzibar mshindi wa Pili Afrika

Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar kwa soka la ufukweni (Sand Heroes) kimerejea visiwani Zanzibar na kombe la ushindi wa pili kwenye mashindano ya Afrika ya soka la ufukweni yaliofanyika nchini Kenya kuanzia Disemba 18 mpaka Disemba 20 Disemba.

Katika mashindano hayo Zanzibar Sand Heroes imeshinda nafasi ya pili kufuatia kufungwa kwenye fainali na timu ya Kenya “A” kwa jumla ya mabao 10-9.
Katika taarifa yake Kocha msaidizi wa timu hiyo Kijo Nadir Nyoni amese walikuwa na uwezo mkubwa wa kurudi na kombe lakini si bahati yao lakini wanajipanga tena kuweza kuitangaza Zanzibar na kuonyesha kuwa wanaweza kuwakilisha.
Hata hivyo Kijo alielezea siri ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ambapo alisema wazanzibar wanaoishi Kenya waliwaunga mkono sana na kuishangilia timu yao.
Mbali ya timu hiyo kupata ushindi wa pili, pia wametoa mchezaji bora kwenye mashindano hayo ambapo alikuwa ni Talib Ame pia alifanikiwa kufunga mabao 14 na kuzawadiwa medali ya dhahabu.

No comments:

Post a Comment