
Jeshi
la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wanne wakiwemo mke wa
marehemu dereva na mtunza bustani kwa tuhuma za mauaji ya aliekuwa mkuu
wa kitengo cha ulinzi na usalama wa shirika la hifadhi za Tanapa Emili
Kisamo aliyeuwawa kwa kukatwa shingo na kutelekezwa ndani ya gari lake
Nissan Mazda No T 435 CSY eneo la Lemala jijini Arusha tarehe kumi na
nane ya mwezi huu.
Kamanda Polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema baada ya
tukio hilo jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kuwakamata watu hao
lakini mtunza bustani Ismail Swalehe amekiri kufanya mauajki hayo kwa
tamaa ya fedha kiasi cha shilingi milioni tano na kati ya hizo milioni
nne zimepatikana zikiwa zimefukiwa chini nje ya nyumba ya marehemu na
kudai alimkata shingo kwa panga akiwa sebuleni anakunywa uji ili aweze
kuelekea kazini.
Kamanda Sabas amesema uchunguzi wa jeshi la polisi pia umegundua
panga moja liliokuwa na damu ambalo lilikutwa kwenye stoo ya nyumba ya
marehemu vitu vingine ni taulo nne kitambaa cha mezani suruali ya
mtuhumiwa ambazo zilifichwa kwenye migomba karibu na banda la kuku
nyumbani kwa marehemu ambazo zinadaiwa ndiyo zilizo tumika kupigia deki
baada ya kuuwawa.
No comments:
Post a Comment