TTCL

EQUITY

Sunday, October 26, 2014

Serikali haijachukua hatua za kutosha kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini.

Serikali imetakiwa kuwa makini na kuchukua tahadhari za kutosha kukabiliana na ugonjwa wa Ebola  kwa kuweka vifaa vya kupima na kubaini watu wenye ugonjwa huo hapa nchini kuliko hali ilivyo kwa sasa kupeleka sampuli za watu wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huo nchini kenya. 
Balozi wa majanga Afrika na mwenyekiti cha chama cha NCCR Mageuzi Mh.James Mbatia ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la vunjo na kusema kuwa bado serikali haijachukua hatua za kutosha za kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba athari zake kidunia ni kubwa hususani katika sekta ya utalii ambayo inategemea wageni kutoka nje ya nchi.
 
Amesema ni vema serikali ikaacha kuingiza masuala ya kisiasa katika ugonjwa wa Ebola na kwamba endapo watalii watasikia Tanzania haina maabara ya kupima sampuli za ugonjwa huo athari zake kiuchumi ni kubwa hapa nchini hususani mkoa wa Kilimanjaro ambao unategemea utalii.
 
Kutokana na wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kupata hofu ya ugonjwa huo kufuatia taarifa za uwepo wa mgonjwa anayehisiwa  kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola katika manispaa ya Moshi  wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment