
Hospitali
ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanjaro inakabiliwa na tatizo la vitanda
vya kufanyia upasuaji hali ambayo inazidi kuchangia ongezeko la
msongamano wa wagonjwa wodini huku baadhi ya wagonjwa wakilazimika
kulala kwenye varanda kusubiri huduma.
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya KCMC Prof Giliad Masenga
ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa Blanketi maalumu za wagonjwa
kutoka benki ya Diomond Trust na kuwa vitanda vinavyotumika kwa sasa ni
chakavu.

Amesema idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji ni kubwa na kwamba
vitanda vilivyopo ni vya zamani na kwamba ununuzi wa vitanda hivyo ni
gharama kubwa ambapo kitanda kimoja kinagharaimu zaidi ya shilingi
milioni 40.
Mapema akikabidhi shuka hizo maalumu za wagonjwa 100 zenye thamani
ya shilingi milioni 5 kati ya shuka 2000 zinazohitajika hosptalini hapo
meneja wa benk ya Diomond Trust tawi la Moshi Bw.John Robert amesema
msaada huo ni sehemu ya faida waliyopata na kutokana na kazi
wanayoifanya.
Akizungumzia hali ya msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo
afisa uhusiano wa hospitali ya rufaa ya KCMC Bw.Gabriel Chiseo amesema
tayari wako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa idara ya
wagonjwa wa dharura ambayo inatarajia kuanza kutumika mwezi January
mwakani 2016.
No comments:
Post a Comment