TTCL

EQUITY

Wednesday, March 4, 2015

Tiketi za kielektroniki zasitishwa

Naibu Waziri, Juma Nkamia akiwa katika moja va vikao vya bunge.

Serikali ya Tanzania imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki ( kununua kwa kutumia njia za mitandao) kwenye Uwanja wa mkuu wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 3, 2015 hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura, uamuzi huo umetangazwa leo (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu 60,000 na ndio uwanja wa kisasa zaidi uliojengwa na Serikali kwa ubia na watu wa Jamhuri ya China.Ni moja ya viwanja vinavyotumika kwa ajili ua mechi za ligi kuu na za kimataifa.
TFF , kwa kushirikiana na moja ya benki kuu nchini Tanzania (CRDB), iliamua kuanzisha mfumo wa kununua tiketi kwa mashabiki kwa njia ya mtandao ili kuepusha usumbufu kwa mashabiki wa soka na pia kuzuia tiketi feki au ulanguzi kutoka kwa wachuuzi wa kawaida.
Hata hivyo, zoezi hilo, ambalo lilianzishwa pia katika viwanja vingine tofauti ikiwa kama sehemu ya majaribio, lilipata baadhi ya dosari ndogondogo, kama vile changamoto za mtandao huku baadhi wakilalamika kuwa wanapata usumbufu wanaponunua tiketi ,wakati mwingine aidha kukoseana au kuchelewa kuleta majibu kama muamala umefanikiwa au la.

No comments:

Post a Comment