TTCL

EQUITY

Friday, March 27, 2015

GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI.


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi ili kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Inadaiwa matusi hayo yamesikika na kuonekana katika videos zilizo wekwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana  Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.


Akizungumza nje ya kituo hicho kabla ya kuanza kuhojiwa, Gwajima amekaririwa2 akisema kwamba alichofanya yeye ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake juu ya makubaliano waliyofikia katika tamko lao linalowahamasisha waumini wao kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa. 

Gwajima, anasema mbali na hilo la Katiba Inayopendekezwa, tamko husika lililotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania, lilipinga kutungwa kwa sheria ya Bunge, chini ya uratibu wa Serikali, inayoruhusu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi. 

“Mimi kama kiongozi wa kiroho niliona nimkemee (Kardinali Pengo) kwa sababu mimi ni Askofu wa Kanisa, na yeye pia ni Askofu wa Kanisa. Ilibidi nimkemee kwamba aache kufanya vile alivyofanya, kuwageuka Maaskofu wenzake,” amekaririwa Gwajima akisema na kuongeza, “Lakini cha msingi ambacho ndicho cha kuwaza niliyemkemea ni Kardinali Pengo au Polisi?” 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alimtaka Gwajima kujisalimisha kuhojiwa kufuatia kusambaa mitandaoni sauti na picha za video zinazomuonyesha akimshambulia kwa maneno makali Kardinali Pengo.


Katika mtandao maarufu wa kijamii nchini, wa JamiiForums kumekuwepo na mijadala mikali juu ya suala hilo ambapo imeripotiwa na mmoja wa wanachama wake aliyejitambulisha kwa jina la Davidm kuwa siku moja baada ya kuitwa na Polisi kujieleza, Gwajima amejitokeza na kujaribu kujitetea kuhusiana na tamko alilolitoa wiki iliyopita akiwa katika Ibada kanisani kwake.

Mwanachama mwingine wa mtandao huo pendwa nchini, aliyejitambulisha kwa jina la East African Eagle, ameandika, “Ule uwanja wa Gwajima si Kanisa, ni eneo la wazi kama ulivyo Uwanja wa Jangwani…si jengo la kanisa lile…kamtukana Askofu Pengo kwenye uwanja wa wazi mbele ya watu wenye dini na wasio na dini kwenye eneo lisilokuwa la kidini, kwenye viwanja vya Tanganyika Packers visivyokuwa vya kidini.
Alitumia jukwaa lile kumtukana Pengo akijua fika kuwa Askofu Pengo si muumini wa kanisa lake wala si kiongozi aliye chini yake, akaamua kumporomoshea matusi ya nguoni wakati akjijua mhusika hakuwemo kanisani kwake.”

No comments:

Post a Comment