TTCL

EQUITY

Friday, March 27, 2015

BARAZA LA KILIMO MLIKUA WAPI ACT WALIPOANZA?

WAKATI Chama Cha siasa Cha Aliance For Chance and Transparency Tanzania (ACT) kikijiandaa kufanya uchaguzi wake mkuu Machi 29 mwaka huu, Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) limekitaka Chama hicho kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwisha sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.



Akizungumza katika kipindi cha Hotmix cha EATV kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa 2:00 jioni, Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt. Sinare Yusuf Sinare amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.

“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare.


Kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi yetu, Jumuiya, Chama ama Taasisi yoyote kisheria hairuhusiwi kujisajili kwanamna yoyote kwa kutumia jina la mtu mwingine ama chombo kilichokwisha sajiliwa, ni kosa kisheria.
kisheria kuna taratibu za kuweka zuio na kukifungia chama kinachobainika kuenenda kinyume na utaratibu, lakini chama cha ACT hadi sasa kimechukua muda mrefu zaidi tangu kusajiliwa kwake.
Mnamo tarehe 14 Dec 2014 ulifanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi  ngazi ya serikali za mitaa Tanzania Bara, na Chama cha ACT - Maendeleo kilikua miongoni mwa chama cha upinzani kilicho simamisha wagombea katika maeneo mbalimbali. Ukiacha na baadhi ya changamoto zilizojitokeza kwenye maeneo ambayo uchaguzi uliahirishwa kwa kukosekana vitendea kazi au kukosewa kwa karatasi za kupigia kura na baadaeye kurudiwa upya.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania toka kuingia katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Vyama vya upinzani vimetoa ushindani na kuweza kushinda maeneo mengi katika uchaguzi huo uliogubikwa na vurugu za hapa na pale.
Aidha Matokeo hayo yanaonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kimeongoza uchaguzi huo kwa kujinyakulia vijiji 7,290 tu sawa na 80.58% na mitaa 2,116 sawa na asilimia 68.7% huku chama kikuu cha upinzani CHADEMA kikijinyakulia vijiji 1,248 sawa na 13.8% na mitaa 753 sawa na 24.5%.
Chama cha Wananchi CUF kiliibuka nafasi ya Tatu kwa kujinyakulia vijiji 382 na mitaa 235 wakati NCCR Mageuzi kikipata mitaa 8, ACT mitaa 9, TLP mtaa 1 na vijiji 2, UDP Vijiji 4 na NLD vijiji 2.
Mikoa ambayo imefanya uchaguzi bila kuwepo kwa kasoro yoyote ni pamoja na Arusha, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Dodoma, Katavi, Kagera na mingine ni Mbeya, Singida na Njombe.
Hadi kufikia hatua hii, kusimamisha wagombea katika mitaa, vijiji na vitongoji na kuweza kujizolea viti 9 ni hatu kubwa na ilikuwepo ridhaa ya msajili wa vyama ili kufanikisha zoezi hili kufanikiwa.
leo baada yakuonekana chama kinapeperusha bindera, kinakuja na sera ya kidemokrasia ndio wanaibuka watu na kusema wameibiwa jina, swali langu ni kwamba walikuwa wapi wakati wa usajili wa chama hichi, lakini pia chama kilipo simamisha wagombea hadi matokeo kutangazwa kwanini hapakuwepo zuio, au hawa wagombea wanatokana na chama cha BARAZA LA KILIMO?
watanzania ni watu makini, tunaishi kwa mujibu wa demokrasia, inafaa kila jambo lililo halali kufanyika kwa uhalali wake na sio vinginevyo, hatutakikuburuzwa na mawazo, tunataka kuendeshwa na maendeleo.

No comments:

Post a Comment